18 July 2016

Jukumu La Kulea Yatima


Watoto wengi wanaojikuta katika wimbi la yatima na kujikuta wanaishia mitaani ni kutokana na kunyanyaswa na wazazi au walezi wao mateso yanayowafanya kujikuta wakiishia mitaani na kuishia katika mateso makali yenye uchungu pasipo msaada.

 


Tukumbuke watoto wengi tunaowaona mitaaani au wakizunguka zunguka barabarani na kulla jalalani ni kwasababu ya kuosa misaada na matunzo wanayohitaji ili waweze kuishi, wapo waliotelekezwa, wapo waliofiwa na wazazi wao kwa sababu tofauti, wapo waliotupwa baada ya kuzaliwa, na wengine ambao wako mitaani kutokana na matatizo ya familia.

Suala la malezi ni jambo la wajibu katika jamii yetu, kwani mtu akosapo malezi ya usawa bila ya shaka atakengeuka na atapotea, na matokeo yake ni kuongeza kundi la watoto wa mitaani na kwa maana hiyo ndiyo jamii ikawapa mzazi au mlezi wajibu wa kumhifadhi na kumlinda mtoto ili asiangamie:

Katika Suala la kulea yatima tutambue kuwa hili ni jukumu zaidi kwani kulea yatima kuna fadhila nyingi na baraka zake ni kubwa mno. Na kutomlea vizuri pia kuna hatari yake.


 Madhara yanayowapata Yatima na watoto wa mitaani

1. UNYANYASAJI


watoto wengi wananyanyaswa ndani ya nyumba za watu bila kupewa misaada na wanaoishi nao wanajulikana na majirani zao, 

Je? mambo haya ya unyanyasaji wa hawa watoto unakomeshwaje? vipo vyombo vya sheria ambavyo vinasimama kutetea haki za watoto na kuwatetea, na ndio maana sisi kama Faharo Foundation tukajikita katika kusaidiana na Organization Nyingine katika kuyafumbua haya na kuwasaidia watoto hawa wanaonyanyaswa ndani ya jamii zetu
 
2. AJIRA ZA UTOTONI

 


Sheria za nchi haziruhusu kabisa ajira za utotoni, jamii nyingi zimekua zikiwafanya watoto kama wafanyakazi wasaidizi katika shughulizao jambo ambalo ni kinyume kabisa na haki za watoto, watoto wanaohitaji malezi bora katika ukuaji wao lakini wamegeuzwa vibaraka na kufanywa kama watumwa,

wasichana wadogo wamekua kama wafanyakazi wa ndani wanaonyanyaswa na kufanyishwa kazi ngumu zilizowazidi uwezo hii inauma sana unapomuona mtoto mdogo akitetea uhai wake pindi anapotakiwa kuvumilia kwa kukosa utetezi wa haki zake.

Usiwe mstari wa nyuma kuyafumbia macho mambo haya katika jamii pinga ajira za watoto au wasilisha maovu haya katika vyombo husika, Fahari Foundation itaungana nawe katika kulitokomeza na kuwaokoa watoto hawa wanaopewa majukumu ambayo si ya kwao, tusiwafanya watoto kama wanyama kisa wamekosa wazazi wao, wazazi waliobaki ni mimi na wewe tuwalee na tuwatunze lakini si kwa kuwatumikisha NO AJIRA ZA UTOTONI.


Hawa ni watoto waliofiwa na wazazi wao wapo tu wanalelewa na ndugu na watu baki, ni mabinti wenye umri wa miaka minne (4) mpaka Sita (6) unadhani hii ni haki yao kubeba matofari na kufanya kazi za ujenzi? Unadhani ni haki kwa mtoto huyu kufanyishwa unyama huu? Je? unaweza kufikiri malipo ya mtoto huyu ni yapi? hatma ya mtoto huyu ni mabaya kama hatutajikita na kutokomeza mambo haya, tunakuomba wewe msamaria mwema kuisaidia Fahari Foundation katika kulifikisha Taifa katika uhuru wa watoto hawa.


3. KUBAKWA / KULAWITIWA



Huyu binti ana miaka tisa, anadai baba yake amekuwa akimuingilia au kumbaka mara kwa mara...

anadai hayo yamemtokea baada ya baba yake kumtimua mama yake na mama kurudi kijijini....

kwa ukatili huu yampasa sasa baba huyo kukamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi, mama na mtoto wamebaki wakiwa na hofu kubwa sana na mama anataka aende kijijini kwao maana hana ndugu hapa mjini ili akae na mwanae... 

wasiwasi wake endapo huyo baba ataachiwa kwa dhamana hakika atawaua kwa sababu huyu mama anadai kwamba huyo baba amekuwa akimtesa kwa miaka mingi mnooo ila kwa hili anahofia atamfanya vibaya sana....

hii ni changamoto kwa jamii na wadau na Serikali, tunahitaji nyumba salama za kuwahifadhi wahanga wa Ukatili kama hawa ili kutoa nafasi nzuri katika kuendesha kesi za namna hii.....

hii ni habari nzito sana tena ni ya kusikitisha kwa mtoto wa miaka tisa (9) kuingiliwa na baba yake mzazi, yatupasa kuwashirikisha mamlaka zinazohusika haraka iwezekanavyo pindi tunapogundua ukatili huu ukiendelea katika jamii na familia zetu, Ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi ili kuweza kulipatia ufumbuzi wa kina.....

Endelea kutembelea ukurasa wetu kwa utambuzi na misaada juu ya taarifa zaidi kuhusiana na yatima na watoto wa mitaani……


4. KUJIINGIZA KATIKA MADAWA YA KULEVYA


Kwa kukosa malezi bora na yasiyo na mwelekeo vijana wengi baadaya ya manyanyaso na ugumu wa maisha ya mitaani hupoteza mwelekeo na kujikuta wakiingia katika makundi yasiofaa, mara nyingi hujikita katika maadili yasiofaa na kufikia hatua ya kua vibaka na kuvuta bangu kuvuta unga n ahata kuingia katika janga bay asana la maambukizi ya maradhi makubwa kama HIV/AIDS sisi kama Jamii yatupasa kuyatazama haya kwa macho matatu ili tuweze kuwasaidia hawa na kuwaepusha katika mitihani hii. 

 5. UKAHABA


***watoto wa namna hii wapo mtaani kwako.. wapo watoto wanaonyanyasika na kuzurura mitaani bila kupata msaada, usiwaangalie na kuwaacha tu hebu jaribu KUWA SAUTI YAO. hawawezi kusema hebu SEMA BADALA YAO. wanalia KISIKIE KILIO CHAO. Jamii ingekua na Moyo wa Huruma juu ya watoto yatima, Tusingekua na watoto wa Mitaa, Vitendo vya kudhalillisha hufanywa sana, Lakin Jamii inachukulia kama haioni

 6. MIMBA NDOA ZA UTOTONI


***watoto wa namna hii wapo mtaani kwako.. wapo watoto wanaonyanyasika na kuzurura mitaani bila kupata msaada, usiwaangalie na kuwaacha tu hebu jaribu KUWA SAUTI YAO. hawawezi kusema hebu SEMA BADALA YAO. wanalia KISIKIE KILIO CHAO. Jamii ingekua na Moyo wa Huruma juu ya watoto yatima, Tusingekua na watoto wa Mitaa, Vitendo vya kudhalillisha hufanywa sana, Lakin Jamii inachukulia kama haioni***