Watoto wengi wanaojikuta katika
wimbi la yatima na kujikuta wanaishia mitaani ni kutokana na kunyanyaswa na
wazazi au walezi wao mateso yanayowafanya kujikuta wakiishia mitaani na kuishia
katika mateso makali yenye uchungu pasipo msaada.
Tukumbuke watoto wengi tunaowaona
mitaaani au wakizunguka zunguka barabarani na kulla jalalani ni kwasababu ya
kuosa misaada na matunzo wanayohitaji ili waweze kuishi, wapo waliotelekezwa,
wapo waliofiwa na wazazi wao kwa sababu tofauti, wapo waliotupwa baada ya
kuzaliwa, na wengine ambao wako mitaani kutokana na matatizo ya familia.
Suala la malezi ni jambo la
wajibu katika jamii yetu, kwani mtu akosapo malezi ya usawa bila ya shaka
atakengeuka na atapotea, na matokeo yake ni kuongeza kundi la watoto wa mitaani
na kwa maana hiyo ndiyo jamii ikawapa mzazi au mlezi wajibu wa kumhifadhi na
kumlinda mtoto ili asiangamie:
Katika Suala la kulea yatima
tutambue kuwa hili ni jukumu zaidi kwani kulea yatima kuna fadhila nyingi na
baraka zake ni kubwa mno. Na kutomlea vizuri pia kuna hatari yake.
Madhara yanayowapata Yatima na
watoto wa mitaani
watoto wengi wananyanyaswa ndani
ya nyumba za watu bila kupewa misaada na wanaoishi nao wanajulikana na majirani
zao,
Je? mambo haya ya unyanyasaji wa
hawa watoto unakomeshwaje? vipo vyombo vya sheria ambavyo vinasimama kutetea
haki za watoto na kuwatetea, na ndio maana sisi kama Faharo Foundation
tukajikita katika kusaidiana na Organization Nyingine katika kuyafumbua haya na
kuwasaidia watoto hawa wanaonyanyaswa ndani ya jamii zetu
2. AJIRA ZA UTOTONI
Sheria za nchi haziruhusu kabisa
ajira za utotoni, jamii nyingi zimekua zikiwafanya watoto kama wafanyakazi
wasaidizi katika shughulizao jambo ambalo ni kinyume kabisa na haki za watoto,
watoto wanaohitaji malezi bora katika ukuaji wao lakini wamegeuzwa vibaraka na
kufanywa kama watumwa,
wasichana wadogo wamekua kama
wafanyakazi wa ndani wanaonyanyaswa na kufanyishwa kazi ngumu zilizowazidi
uwezo hii inauma sana unapomuona mtoto mdogo akitetea uhai wake pindi
anapotakiwa kuvumilia kwa kukosa utetezi wa haki zake.
Usiwe mstari wa nyuma kuyafumbia
macho mambo haya katika jamii pinga ajira za watoto au wasilisha maovu haya
katika vyombo husika, Fahari Foundation itaungana nawe katika kulitokomeza na
kuwaokoa watoto hawa wanaopewa majukumu ambayo si ya kwao, tusiwafanya watoto
kama wanyama kisa wamekosa wazazi wao, wazazi waliobaki ni mimi na wewe tuwalee
na tuwatunze lakini si kwa kuwatumikisha NO AJIRA ZA UTOTONI.
Hawa ni watoto waliofiwa na
wazazi wao wapo tu wanalelewa na ndugu na watu baki, ni mabinti wenye umri wa
miaka minne (4) mpaka Sita (6) unadhani hii ni haki yao kubeba matofari na
kufanya kazi za ujenzi? Unadhani ni haki kwa mtoto huyu kufanyishwa unyama huu?
Je? unaweza kufikiri malipo ya mtoto huyu ni yapi? hatma ya mtoto huyu ni
mabaya kama hatutajikita na kutokomeza mambo haya, tunakuomba wewe msamaria
mwema kuisaidia Fahari Foundation katika kulifikisha Taifa katika uhuru wa watoto
hawa.
3. KUBAKWA / KULAWITIWA
Huyu
binti ana miaka tisa, anadai baba yake amekuwa akimuingilia au kumbaka mara kwa
mara...
anadai
hayo yamemtokea baada ya baba yake kumtimua mama yake na mama kurudi
kijijini....
kwa
ukatili huu yampasa sasa baba huyo kukamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi,
mama na mtoto wamebaki wakiwa na hofu kubwa sana na mama anataka aende kijijini
kwao maana hana ndugu hapa mjini ili akae na mwanae...
wasiwasi
wake endapo huyo baba ataachiwa kwa dhamana hakika atawaua kwa sababu huyu mama
anadai kwamba huyo baba amekuwa akimtesa kwa miaka mingi mnooo ila kwa hili
anahofia atamfanya vibaya sana....
hii
ni changamoto kwa jamii na wadau na Serikali, tunahitaji nyumba salama za
kuwahifadhi wahanga wa Ukatili kama hawa ili kutoa nafasi nzuri katika
kuendesha kesi za namna hii.....
hii
ni habari nzito sana tena ni ya kusikitisha kwa mtoto wa miaka tisa (9)
kuingiliwa na baba yake mzazi, yatupasa kuwashirikisha mamlaka zinazohusika haraka
iwezekanavyo pindi tunapogundua ukatili huu ukiendelea katika jamii na familia
zetu, Ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi ili kuweza kulipatia ufumbuzi
wa kina.....
Endelea kutembelea ukurasa wetu kwa utambuzi na misaada juu ya taarifa
zaidi kuhusiana na yatima na watoto wa mitaani……
Kwa kukosa malezi bora na yasiyo
na mwelekeo vijana wengi baadaya ya manyanyaso na ugumu wa maisha ya mitaani
hupoteza mwelekeo na kujikuta wakiingia katika makundi yasiofaa, mara nyingi
hujikita katika maadili yasiofaa na kufikia hatua ya kua vibaka na kuvuta bangu
kuvuta unga n ahata kuingia katika janga bay asana la maambukizi ya maradhi
makubwa kama HIV/AIDS sisi kama Jamii yatupasa kuyatazama haya kwa macho matatu
ili tuweze kuwasaidia hawa na kuwaepusha katika mitihani hii.
5. UKAHABA
***watoto wa namna hii wapo
mtaani kwako.. wapo watoto wanaonyanyasika na kuzurura mitaani bila kupata
msaada, usiwaangalie na kuwaacha tu hebu
jaribu KUWA
SAUTI YAO. hawawezi kusema hebu
SEMA BADALA
YAO. wanalia KISIKIE KILIO CHAO. Jamii ingekua na Moyo wa
Huruma juu ya watoto yatima, Tusingekua na watoto wa Mitaa, Vitendo vya
kudhalillisha hufanywa sana, Lakin Jamii inachukulia kama haioni
***watoto wa namna hii wapo
mtaani kwako.. wapo watoto wanaonyanyasika na kuzurura mitaani bila kupata
msaada, usiwaangalie na kuwaacha tu hebu
jaribu KUWA
SAUTI YAO. hawawezi kusema hebu
SEMA BADALA
YAO. wanalia KISIKIE KILIO CHAO. Jamii ingekua na Moyo wa
Huruma juu ya watoto yatima, Tusingekua na watoto wa Mitaa, Vitendo vya
kudhalillisha hufanywa sana, Lakin Jamii inachukulia kama haioni***






