TUWASAIDIE WATOTO
WENYE MAHITAJI MAALUMU, NI WATOTO WETU NA WADOGO ZETU
Tunapozungumzia watoto wa mitaani kila
mtu ana uelewa wake juu ya hilo na kwa muonekano anao uona yeye,
MTOTO WA MTAANI:
Ni mtoto
ambaye anayeishi katika mazingira ya kutangatanga mitaani bila ya kuwa na
sehemu maalumu ya kuishi na kutopata mahitaji muhimu anayotakiwa kupata
mwanadamu,
Kama
vile chakula,maradhi na nguo.
Tunapoangalia kwa muono wetu watoto wa mtaani wako wa aina tofauti tofauti na
wamekuwa watoto wa mtaani kwa sababu tofauti tofauti.
Kila mtu ana historia yake katika
maisha ama mbaya au nzuri ya enzi za utoto wake, wapo ambao wakikumbuka nyuma
wanalia na kuichukia dunia maana walikosa tumaini na faraja toka utotoni mwao.
Leo hii sisi tuliokwisha ona angalau mwanga katika hii dunia ni vyema tukawa
tumaini au faraja nzuri kwa watoto wote wenye mahitaji maalumu katika jamii,
tukiwasaidia kuanzia malezi bora, elimu bora lakini pia kunyanyua na kuvumbua
vipaji vyao ili kuvikuza waje kuwa zao jema ukubwani, wasije wakalia na
kuichukia dunia kama wengine, ni jukumu letu kama jamii, kujali, kuthamini na
kutambua wajibu wetu kwa hawa watoto.
Kuna makundi mbalimbali ya
watoto ambao bila kujitoa kwetu kwa ajili yao ni sawa na kuandaa kizazi ambacho
kwao furaha na upendo vitakuwa ni vitu vya kuvisikia kwa wengine, pia ni sawa
na kuandaa kizazi chenye chuki na hasira na matokeo yake ni kujiingiza katika
vitendo visivyo vya kiungwana.
MTOTO WA MTAANI ANAYETOKANA NA
KUFIWA NA WAZAZI:
Huyu ni mtoto ambaye aliyekuwa akilelewa malezi yote anayestahiki kupewa mtoto na katika mstari uliokuwa sahihi.
Huyu ni mtoto ambaye aliyekuwa akilelewa malezi yote anayestahiki kupewa mtoto na katika mstari uliokuwa sahihi.

Mara nyingi watoto wa aina hii pindi wanapofiwa na wazazi
huwa wanapitia tabu nyingi sana na kuwapelekea kuwa watoto wa mitaani, Pindi tu
pale wanapofiwa na wazazi ndugu wenye tama za mali ujifanya wanapenda kukaa na
watoto wa aina hii na kuwanyanyasa katika mali za wazazi wao na mwisho wake ni
kuwafukuza katika majumba wanayoacha wazazi wao,
ENYI WAZAZI/WALEZI: mnawachukua
watoto wa ndugu zenu kwa kuwataka kuwalea kwa tama za mali tu na si kwa mapenzi ya
dhati,sasa tubadilike na tuseme inatosha.
Kuondokewa kwa wazazi si mwanzo wa mtoto kuitwa mtoto wa mtaani na kupata mateso makubwa ambayo hayastahili, tuwapende watoto wa ndugu zetu na tuwalee kwa moyo mkunjufu na wa upendo, hakika Mungu atawalipa mema tu
Kuondokewa kwa wazazi si mwanzo wa mtoto kuitwa mtoto wa mtaani na kupata mateso makubwa ambayo hayastahili, tuwapende watoto wa ndugu zetu na tuwalee kwa moyo mkunjufu na wa upendo, hakika Mungu atawalipa mema tu
MTOTO WA MTAANI ANAYETOKANA NA
KUTELEKEZWA NA MZAZI/MLEZI:
huyu ni
mtoto wa mtaani anayesababishiwa na mzazi au mlezi mwenyewe kuitwa mtoto wa
mtaani, Utakuta mzazi au mlezi amemzaa mtoto vizuri na akawa ana mlea lea
lakini baadae akaona maisha magumu au ana taka arudi tena kwenye ujana kama
mwanzo, mambo haya uwaga wanafanya sana WANAWAKE kama ulikuwa unaona maisha
magumu ulikubali vipi kuzaaa au unataka uwe kijana kila siku, mnaona
mtelekeze watoto pahali popote pale na kuwakimbia kwa kuwadanganya utarudi
kumbe ndo kwa kheri, kina mama tubadilike tuwe na mioyo ya uruma kwa watoto
wetu na kuwapenda kwa hali yoyote ile,kama ulivyomuweka tumboni miezi tisa na
ukamzaa kwa uchungu.
WANAUME: kina
baba wengi upenda kutelekeza familia zao zikitanga tanga ovyo bila ya sababu za
msingi mitaani, na kuwapelekea watoto kuitwa watoto wa mitaani kwa kukosa
mahitaji muhimu sana sana maradhi mtoto hata njiani analala hana sehemu ya
kuishi
Watoto hawa wanaotokana na kutelekezwa
wanasikitisha sana katika jamii, wazazi na walezi wa pande mbili wanaume na
wanawake, tujitahidi katika malezi ya watoto wetu, tusiwaache kwa kuwatelekeza
wakawa watoto wa mitahani tunaopofanya maamuzi yufikirie mara mbili mbili
maamuzi yetu, wazazi wa pande mbili wote tushirikiane ili kupunguza
ongezeko la watoto wa mitaani, tumuogopeni MUNGU tutaenda jibu nini kesho
kwake, wazazi tujitaidi kuwalea watoto wetu na tuache tabia ya kutelekeza
watoto wasiokua na kosa.
WATOTO WA MITAANI WANAOTOKA MKOA
MMOJA KWENDA MWINGINE:
Watoto
wa mitaani hawa ni wale wanaochukuliwa mikoani kwa lkudanganywa wanakuja
kusomeshwa na watu ambao wanawachukua, kumbe lengo kubwa la watu wengi
wanaowagiza watoto kutoka mikoani au kuwafuata vijijini kwa kuwa labda wanatoka
kijiji kimoja lengo lao kubwa ni kuja kuwafanyisha kazi watoto wa watu na
kuwatesa na kuwafukuza kama mbwa na kuwaacha wakitanga mitaani kwa kuwa
awana ndugu wala jamaaa mkoa walopelekwa,japo kuna wengine wanaokaa na
watoto wa watu vizuri mungu awazidishie.
ENYI WAZAZI: mnaotoa
watoto wenu ovyo kwa tamaaa labda ya vijihela mbadilike na muwapende watoto
wenu msipende wakawa watoto wa mitaani na hali ya kuwa wazazi mpo hai, na kwa
NYIE mnaowachukua watoto wa wenzenu na kuwaleta mikoa mingine kuweni na roho za
huruma jamani na muwapende watoto wa wenzenu mtoto wa mwenzio ni mtoto wako pia,
JAMII KWA UJUMLA: Tumeona
watoto wa MITAANI wanapatikana kwa njia tofauti tofauti, wewe kama mzazi au
mlezi au mtanzania na una uzarendo na nchi yako tujitaidi kuwaangalia kwa jicho
la umakini na la uruma watoto wetu wa MITAAN. na tuwe kipau mbele kuwasaidia na
kuwatunza katika jamiii yetu, tuachane na fikra na mawazo potofu na
tuache tabia ya kuwatenga tukawaacha bila msaada.
SERIKALI: Ijitaidi
kujenga mashule mengi ili kuepukana na watoto wa MITAANI na kuweza
kuongeza Vituo vya kuwalea watoto hawa wa mtaani, pia ituwezeshe mashirika
ua taasisi zinazosapoti jitihada hizi za kuwasaidia watoto hawa Yatima na
watoto wa mitaani.
Mtanzania kuwa mzarendo na kuwa na huruma kwa WATOTO WETU WA MITAANI,
tunakuhitaji wewe mtanzania Pamoja na Fahari Foundation tushirikiane kwa pamoja kupunguza ongezeko la watoto wetu yatima
na watoto wa mtaani.
JAMII IWAJIBIKE KUWASAIDIA WATOTO WA MITAANI, YATIMA
Kitanda
usichokilalia, huwezi kujua kunguni wake, shida na mateso wanayoyapata watoto
waishio katika mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kueleza. Watoto
hawa hawajui leo au kesho yao watakula nini, hakuna anayeangaika kuwatafutia
chakula, wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia, na wakiumwa hakuna wa kumweleza,
hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona kabisa.
Ukweli ni kwamba, watoto hawa
hujisikia wapweke na wenye kudhoofika moyini kutokana na jamii kubwa kuwakataa
na kuwaweka katika fungu tofauti. Jambo la kusikitisha, idadi kubwa ya watoto
hawa ni kwamba umri wao unaanzia miaka miwili (2) hadi kumi (10), ambao
kimsingi hawajui kujitegemea, njaa ikiuma wanalia tu bila tegemezi wala msaada
na kushindwa kujieleza.
Kitanda chao ni barabarani na wengine huona
msaada wao ni kulala mitaroni, baridi yote ya usiku na jua la mchana ni lao, hawajui
kubadilisha nguo zao, zile walizovaa wiki kadhaa zilizopita hadi leo hazijatoka
mwilini mwao, Tumezowea kuwaona watoto wenye wazazi wakitoka nyumbani asubuhi na
wazazi wao na kurudi majumbani mwao jioni wakiwa wamenawiri na wenye Amani na
furaha.
Watoto hawa yatima na wanaoishi
katika mazingira hatarishi hawana pa kwenda, popote wanalala, chochote wanakula,
hawana zuri wanalokutana nao, Jamii imesahau kuwa watoto hawa ni sawa na wao,
wanasikia njaa kama watoto wao, baridi na maumivu sawa na wenzao, lakini nani
anashughulika nao?
Fahari Foundation Imeliona
hili na inakuomba wewe ushirikiane nasi ili kuwasaidia yatima hawa kuwarudishia
furaha yao, Amani yao, kwa kuwatoka katika maumivu makubwa na mateso ya usiku
na mchana, kuwapa mahali pa kulala, chakula, mavazi, matibabu na hata elimu.
Tukumbuke kua Watoto hawa
hawakuchagua kuwa yatima na kuishi mitaani, na wala hawakuchagua kufiwa na
wazazi wao na wala hawakupenda kutelekezwa na wazazi au walezi wao, wamejikuta
wapo mitaani na hawana la kufanya kama watoto wetu wanavyojikuta wakiwa
mikononi mwetu na wanapata kila kitu. Wahenga wanasema, kinga ni bora kuliko
tiba.
Fahari Foundation Kushirikiana
na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO`s) na yale ya kimataifa na Serikali, kwa
Pamoja tunasisitiza kushughulikia tatizo la watoto hawa wakiwa tayari mitaani.
Jambo la msingi, nguvu inayotumika kuwasaidia watoto hawa ingepaswa kuelekezwa
kwenye kinga ili kutibu tatizo hilo kabisa.
Sababu moja wapo inayochangia
ongezeko la yatima na watoto wa mitaani ni migogoro isiyokwisha katika ndoa,
Manyanyaso ya kijinsia, ubaguzi wa watoto, Pamoja na unyanyasaji wa kijinsia,
mila n.k
Hatua za haraka zinahitajika ili
kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wa mitaani na yatima kwa kuwaunganisha
na walezi pamoja na ndugu zao ambao tunaamini wapo.
Umefika wakati wa serikali kuratibu
nguvu za mashirika haya na NGOs kwa kuhakikisha mashirika hayo, jamii na wao
wenyewe wanachukua hatua stahiki kuhakikisha tatizo hilo nchini linakwisha...
Fahari Foundation inachukua
mstari wa mbele kuwatetea watoto hawa walio katika hatari kubwa ya maisha yao
wasipojua kesho yao, Kula kwao, kulala kwako kwa shida na taabu, kuugua kwao.
MIMI, WEWE NA YULE
TUWE SEHEMU YA FURAHA KWA HAWA WATOTO.
Miaka
takribani saba iliyopita kwenye mtaa fulani hapa Nchini katika usiku wa giza zito
uliofunikwa na baridi kali iliyochangamana na ukungu, wapo vijana kadhaa
wamelala chini ya mitaro, wamesogeleana karibu ili angalau wapate joto katika
miili yao. Mashuka yao ni maboksi yaliyotolewa vitu vya thamani na kutupwa
jalalani.
Kati
ya vijana hawa ambao wamelala chini ya moja ya mitaro nilikuwepo mimi
nimesimama pembeni yao ambapo kabla ya miaka saba iliyopita nilikuwa nikiishi
nyumbani kwetu Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Huko
nilikuwa nikiishi na wazazi wangu wote wawili, lakini baadaye wazazi wangu
waliachana kufuatia kutokuwepo maelewano baina yao. Baba yangu akahamia Njombe
na mama yangu akabakia Ifakara.
“Baada
ya wazazi wangu kuachana maisha yalikuwa magumu pale nyumbani Ifakara hivyo
mama akanishauri nimfuate baba hapa Njombe, nilifika Njombe na kuonana na baba
yangu ambaye tayari alikuwa ameoa mke mwingine”, anasema Kijana huyo.
Maisha
yangu na mama mpya hayakwenda vizuri kwani mama huyo hakunipenda. Chuki, kazi
nyingi na kugombezwa zikanifanya baba mzazi kutafuta chumba maeneo ya Mgendera
na kunipangishia mwanaye. Aliendelea kuhadithia kijana huyo.
Kama
walivyo wazazi wengine wasiojali, baba yake akaanza kumtelekeza kijana wake
taratibu na hatimaye mawasiliano kati yao yakafa kabisa. Shida nyingi zikamfika
kijana huyo na moja ya shida hizo ni chakula na pango la nyumba.
“Nakumbuka
baada ya baba kunitelekeza maisha yakabana zaidi, hapo ikabidi niwe naelekea
mjini kutafuta kazi ambazo pia sikupata hali iliyopelekea kufukuzwa katika
chumba alichokuwa amenipangia baba huku mwenye nyumba akaninyanganya kitanda
ili kufidia kodi yake.” Aliendelea kusema kijana huyo.
Baada
ya kuwa amefukuzwa katika chumba alichokuwa akiishi Kijana huyo aliamua kuingia
mtaani, akawa mmoja wa watoto wa mtaani, huko maisha mapya ya ubabe, utumiaji
madawa ya kulevya, Ulawiti, kesi za kusingiziwa wizi, kuomba kwa wapita njia,
na kufukua jalalani akitafuta chakula na vyuma chakavu ikawa sehemu yake ya
maisha.
“Maisha
ya mtaani yalikuwa machungu zaidi ya kifo unachokijua. kila siku mimi na watoto
wengine walionikaribisha mtaani tulizurura kila kona tukitafuta chakula, mavazi
na malazi… nilijawa hofu sana, sikuwa na raha Zaidi ya wasiwasi mwingi
ulizunguka maisha yangu.. lakini ningefanya nini!? Hapana, sikuwa na namna ya
kufanya… nilijipa moyo nikajikaza kiume na kuendelea na maisha”.
Nilichojifunza
kikubwa ni kwamba mitazamo hasi ya jamii kuhusu watoto wa mitaani mara nyingi
imekuwa chachu ya kufanya maisha ya watoto hawa kuwa magumu na hivyo
kuwalazimisha kufanya matukio mengine ambayo katika maisha yao hawakuwahi
kufikiria kuyafanya.
Kijana
huyu anabainisha wazi kwamba ipo sehemu ya jamii inawaona watoto wa mtaani kama
nuksi, vibaka, wabakaji. Na kwa sababu hiyo wameamua kuwapa mgongo.
“Kwa
kuwa jamii na serikali imetutenga hii inakuwa fursa ya wakora wengine
kututendea watoto wa mitaani matendo maovu wayatakayo, siku moja tukiwa
tumelala katika moja ya mitaa ya Njombe tulivamiwa na kundi la watu wanaotuzidi
umri wanaonekana kuwa na maisha safi, wakawashika watoto watatu kati yetu mimi
na baadhi ya wenzangu tukakimbia, ajabu wale watu waliwalawiti wale watoto
wenzangu, zingatia kuwa umri wa watoto wenzangu ulikuwa kati ya miaka 10 mpaka
13.”
“katika kipindi nilichokuwa nikiishi mtaani
wapo wachache waliotusaidia sisi watoto wa mtaani, lakini kibaya zaidi wale
ambao mnawaita matajiri, wenye pesa zao na magari ya kifahari hapa Njombe na
wanaoishi kwenye nyumba zilizondani ya kuta za gharama kubwa hakuna hata mmoja
kati ya hao aliyewahi kutusaidia” aliongeza.
Badala
yake kijana huyo aliueleza kuwa msaada mkubwa waliupata kutoka kwa masikini na
watu wenye kipato cha kawaida.
Nilipomuuliza
kuhusu wapi alipo baba yake, hivi ndivyo alivyosema kijana huyo,
“Baada
ya kukaa muda mrefu bila ya kuonana ama kuwasiliana na baba yangu baadaye
nilipata taarifa kuwa alifariki dunia siku nyingi, natamani ningeweza kumuona
japo kwa mara ya mwisho ama kufahamu wapi kaburi lake lilipo niende
kulitembelea lakini haijawa hivyo, kwa hili nasikitika sana.”
Kijana
huyo kwa sasa anaishi katika kituo cha kulea watoto waishio katika mazingira
magumu cha ‘Compasion’ cha Airport mjini Njombe, anakiri na kushukuru kufika
hapo kwani kituo kinamsomesha kwa gharama zake. Hivi sasa yupo kidato cha pili
katika shule ya sekondari ya Mpechi.
Kijana
huyu ni mjuzi pia wa masuala ya umeme pamoja na utengenezaji madishi ya
Luninga, kupitia kipawa alichonacho unaweza kumpa ajira ambayo mwisho wa siku
ikampatia kipato na hivyo kumpa maisha bora.
"Haya
maisha mpaka lini"?
Ni
maneno ya huyu mtoto ambaye hajui atakula nini na atalala wapi?












No comments:
Post a Comment